Nyota wa muziki wa Hip-Hop na filamu nchini Marekani Curtis James Jackson III maarufu kama 50 Cent ametoa sababu za kutofanya vizuri katika muziki akisema kwa sasa amejikita katika uandaaji wa falamu kuliko muziki huku pia akieleza alivyokataa pesa za Donald Trump.

Akiongea na Ebro ambaye ni mtangazaji wa redio ya Hot 97 mjini New York, 50 Cent ameibua siri nzito baada ya kusema alikataa ofa ya Dola laki 5 za kimarekani kutoka kwa Rais wa sasa wa Marekani Donald Trump.

50 Cent amesema kwamba Donald Trump alitaka kumpa ofa ya dola laki tano kwa ajili ya kumsaidia kwenye kampeni yake ya urais, Cent aliendelea kuongeza kwamba Trump alimtaka awashawishi wamarekani weusi kwenda kumpigia kura lakini rapa huyo alikataa kwa kusema pesa hiyo haikuwa na thamani ya jambo hilo.

Tazama alichokiseama 50 Cent katika video hii hapa chini;

Ligi daraja la kwanza kuendelea kesho
Guardiola: Sergio Aguero amepata mpasuko kwenye mbavu