Baada ya Ashanti United na Friends Rangers kuchuana leo Ijumaa, mechi nyingine za ligi hiyo zitaendelea kesho Jumamosi Septemba 30, mwaka huu.

JKT Ruvu na Kiluvya United zinatarajiwa kucheza kesho kwenye Uwanja wa Mbweni katika mchezo wa kundi A kama ilivyokuwa kwa timu ambazo zimecheza leo – Ashanti na Friends.

Kundi B kutakuwa na michezo miwili ambako Mufindi United itacheza na Mlale JKT kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa wakati KMC itacheza na Coastal Union kwenye Uwanja wa Azam, Dar es Salaam.

Kundi C kutakuwa na mchezo mmoja ambako Rhino itacheza na JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

wakati huo huo Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara (SDL), inatarajiwa kuanza Septemba 30, mwaka huu kwa timu kuchuana katika viwanja vitano tofauti.

Kwa mujibu wa Ratiba ambayo imeambatanishwa, michezo ya siku hiyo itakuwa ni kati ya Abajalo na Cosmopolitan; Namungo na Reha kutoka Kundi A wakati kundi B kutakuwa na mchezo kati ya Pepsi na Madini.

Kundi C kutakuwa na mchezo kati ya Burkinafaso na Ihefu kadhalika Boma itacheza na Mkamba Rangers huku Kundi D likikutanisha timu za Bulyanhulu na Milambo.

Katika Kundi hilo la D Mchezo kati ya Nyanza FC na Area C uliokuwa ufanyike Septemba 30, 2017 siku ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, sasa utachezwa Oktoba 01, 2017 siku ya Jumapili kwenye Uwanja huo huo.

Sababu za mabadiliko haya ni kutokana na mchezo kati ya Pepsi FC vs Madini FC kuchezwa tarehe 30.09.2017 katika uwanja huo. Awali mchezo wa Nyanza na Area C ulipangwa kufanyika mkoani Manyara, lakini kutokana na hali ya uwanja ilibidi Bodi ya ligi ufanye mabadiliko husika.

Mpina atoa tano kwa viwanda mkoani Morogoro
Video: 50 Cent aeleza alivyokataa pesa za Trump