Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amekipongeza kiwanda cha nguo cha 21st century na kiwanda cha ngozi cha Ace Leather Tanzania Ltd kwa kutekeleza sheria ya mazingira kwa kujenga mtambo wa kisasa wa kutibu majitaka yanayotoka katika viwanda hivyo.
 
Ameyasema hayo wakati wa Ziara ya ukaguzi na utekelezaji wa sheria ya mazingira mkoani Morogoro, ambapo amewataka wamiliki wa viwanda hivyo kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC pamoja na Bonde la Wami Ruvu, kuchukua Sampuli za maji hayo yanayotibiwa katika viwanda hivyo kwa ajili ya vipimo ili kujiridhisha kama hayana madhara kwa mazingira na viumbe hai wengine.
 
Aidha, katika ziara hiyo Mpina, ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi la Mazingira (NEMC) kuandika barua kwa msajili wa hazina ili kujua ukweli wa mmiliki halali wa mabwawa ya majitaka yaliyotelekezwa katika maeneo ya kilimahewa.
 
  • Tanzania yajipanga kuwa mwenyeji fainali za Afcon
  • Mbunge wa Kilombero akamatwa na Polisi
  • Serikali kujenga vyumba vya upasuaji 170
 
Hata hivyo, ameagiza kujengwa kwa miuondo mbinu kwa mabwawa ya majitaka na kutibiwa kwa maji hayo ili kunususu mazingira na kuondokana na malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na wananchi kuhusu harufu kali ambayo imekuwa ikihatarisha afya zao.

Dkt. Mwakyembe apiga marufuku matumizi ya takwimu GeoPoll
Ligi daraja la kwanza kuendelea kesho