Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amepiga marufuku matumizi ya takwimu zinazotolewa na kampuni ya GeoPoll zinazohusu Kiwango cha wananchi kusikiliza na kutazama vituo vya Redio na Televisheni hapa nchini kwa kuwa takwimu hizo zina mapungufu makubwa.

Ametoa agizo hilo jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kukutana na makampuni ya ukusanyaji na usambazi wa takwimu kwa upande mmoja na watumiaji wa takwimu ambao ni vituo vya Redio na Televisheni.

Katika kikao hicho cha pamoja, makampuni ya IPSOS Tanzania, Push Observer na GeoPoll walifafanya mawasilisho ya namna wanavyokusanya takwimu wakati Ofisi ya Taifa ya Takwimu yenyewe ilifanya wasilisho la kuonyesha njia bora na sahihi za ukusanyaji na usambazaji takwimu.

“Nimeamua kuzuia utumiaji na usambazaji wa takwimu za kampuni ya GeoPoll hapa nchini baada ya kugundua tafiti za hii kampuni zina mapungufu makubwa na kusababisha malalamiko mengi kutoka kwa wadau na wamiliki wa vituo mbalimbali vya radio na televisheni,”amesema Dkt. Mwakyembe

Vile vile, Kutokana na kupigwa marufuku matumizi ya takwimu za GeoPoll nchini, Dkt. Mwakyembe ameyataka makampuni yanayofanya uwakala wa kusambaza matangazo katika vituo vya Televisioni na Redio kusitisha kutumia takwimu za kampuni hiyo kama kigezo cha kutoa matangazo kwa vituo vya Televisheni na Redio.

Aidha Dkt. Mwakyembe amefafanua kuwa kama nchi haiwezi kwenda kwa utaratibu huo, kwani dunia ya leo ni ya biashara na ushindani ni mkubwa ambao unaendana na kujiuza na kujitangaza kwa chombo husika,

Hata hivyo,Dkt. Mwakyembe ameunda kamati ya watu watatu inayohusisha Idara ya Habari (MAELEZO), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pamoja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ambayo itafanyia kazi maoni yaliyotolewa na wadau katika kikao hicho na na mwishoni mwa mwezi wa kumi iwasilishe mapendekezo ya namna bora ya ukusanyaji na usambazaji takwimu kwa mujibu wa sharia na taratibu.

 

Gazeti la Raia Mwema lafungiwa kwa siku 90
Mpina atoa tano kwa viwanda mkoani Morogoro