Klabu ya Manchester City imethibitisha kuwa mshambuliaji wake Sergio Aguero amepata ajali ya gari iliyotokea huko Amsterdam Uhoranzi hapo jana.

Polisi nchini Uhoranzi aliuambia mtandao wa Skysport kwamba katika ajali hiyo watu wawili walijeruhiwa na kupelekwa Hospitali lakini hakutaja majina yao.

Hata hivyo baadae klabu ya Manchester City iliripoti kuwa mshambuliaji wa klabau hiyo Sergio Aguero ni mmoja wa waanga wa ajali hiyo.
Ripoti ya klabu hiyo imesema ”Sergio Aguero atapimwa na madaktari wa klabu leo ​​(Ijumaa)  baada ya kupata ajali ya gari siku ya Alhamisi”
“Atarudi jijini Manchester asubuhi hii na hali yake itafuatiliwa kabla ya mchezo wa Ligi kuu siku ya Jumamosi dhidi ya Chelsea.”
Aguero ambaye mpaka sasa amefunga mabao 6 katika ligi kuu ya Uingereza alikuwa Uhoranzi kwa mapumziko mafupi na alipata ajali hiyo asubuhi akielekea katika uwangja wa ndege ili kwenda jijini Manchester.
Muargentina huyo alipost picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na muimbaji wa Colombia Maluma ikionekana kuwa alihudhuria tamasha ya Maluma kabla ajali hiyo ikitokea.

@maluma . Gracias por la invitación !! ??

A post shared by Sergio Leonel Agüero (@10aguerosergiokun) on

Huyu ndiye kocha wa muda aliyechukua nafasi ya Carlo Ancelotti
Hawa ndio wasanii wa Hip-Hop wanaoingiza pesa nyingi