Michuano ya Uefa Europa Ligi imepigwa usiku wa kuamkia leo kwa michezo mbalimbali katika hatua ya Makundi.

Klabu ya Arsenal ikiwa ugenini imeshinda mabao 4-2 dhidi ya Bate Borisov huku mshambuliaji Olivier Giroud akifunga bao lake la 100 tangu ajiunge na Arsenal, mabao mengine yalifungwa na Theo Walcott aliyefunga mabao 2 na Rob Holding, Mabao ya BAET yalifungwa na Marko Ivanovic na Gordechuk.

Everton imetoka sare ya bao 2-2 na Apollon, Ac Millan imeshinda 3-2 dhidi ya Rijea, Lyon pia wamefanikiwa kutoa sare na Atlanta baada ya kufungana bao 1-1.

Katika mchezo mwangine Nice imeichapa Vitese mabao 3-0, Mainz imefungwa bao 1-0 na Hoffeinheim, Partizan imechapwa na Dynamo magoli 3-2 na Maccab Tel Aviv imetoka sare na Villareal 0-0.

Fc sheriff imetoshana nguvu na Koeben kwa sare ya kutofungana 0-0, Lugan imeambulia kipigo cha bao 2-1 dhidi ya FC FCSB ,Plesen imeichakaza Hapoel bao 3-0.

FC Cologne imefungwa bao 1-0 na FK Crvena Zvezda, Salzburg imeshinda bao 1-0 dhidi ya Marseille, Oestersunds FK imeichapa Hertha Berlin bao 1-0, Konyaspor imetakata kwa ushindi wa bao 2-1 na Vitoria de Guimaraes.

AEK Athens imetoshana nguvu na Austria Wien ya bao kwa kufungana bao 2-2.

Wachezaji 5 watajwa kumfukuzisha kazi Ancelotti
Usalama wa wakimbizi Burundi mashakani