Baada ya Carlo Ancelotti kupoteza ajira yake katika klabu bingwa ya Ujerumani Bayern Munich kutokana mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha, Rais wa klabu hiyo Uli Hoeness ametaja moja ya sababu kuu zilizosababisha uongozi wa Bayern kuamua kumfukuza kocha huyo.

Uli Hoeness anasema kulikuwa na wachezaji wakubwa watano ambao haweakuwa na imani na kocha huyo na walianza kumpinga.

“Kama kocha huwezi kuwa na wachezaji wakubwa kwenye kikosi chako ambao wanakupinga. Nimejifunza hili maisha yangu yote na msemo usemao; Adui aliyepo kitandani kwako ndio hatari zaidi kutokana na jambo hilo ilitubidi kuchukua maamuzi magumu dhidi ya Mr. Ancelotti,” alisema Uli Hoeness.

Carlo Ancelotti akiwa na Bayern Munich ana rekodi ya kuiongoza katika mechi 60 na wameshinda michezo 42, sare 9 na wamepoteza mechi 9. Timu yake ilifunga magoli 156, na pia waliruhusu magoli 50 kutinga kwenye nyavu zao. Ameshinda Bundesliga mara moja na DFL Supercup mara 2.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea, PSG, Real Madrid na AC Milan ameshinda ubingwa wa ulaya mara 3 akiwa na Milan mwaka 2003 na 2007, akashinda La Decimal na Madrid mwaka 2014.

Idadi hii inamfanya kuwa mmoja kati ya makocha wawili waliofanikiwa zaidi katika historia ya michuano ya ulaya sambamba na kocha wa zamani wa Liverpool Bob Paisley, ambaye alishinda ubingwa wa ulaya miaka ya 1977, 1978 na 1981.

TID atangaza nia ya ubunge 2020, aanza kumwaga sera
Giroud apiga bao la 100 Arsenal ikiichapa BATE Borisov