Willy Sagnol ndiye kocha mpya wa Bayern Munich aliyechukua nafasi ya Carlo Ancelotti ambaye ametimuliwa katika klabu hiyo, tofauti na matarajio ya wengi walivyodhani kwamba Bayern wangempa kazi kocha mwingine mwenye jina kubwa klabu hiyo imeamua kumpa timu kwa muda Willy Sagnol ambaye pia matokeo yanaweza kuamua nafasi yake.

Kocha huyo ametumia muda wake mwingi wa soka katika nchi ya Ujerumani lakini sio Mjerumani, Sagnol ni raia wa Ufaransa na alizaliwa huko Saint Etienne Ufaransa mwaka 1977.

Kuanzia mwaka 2000 mpaka 2009 Sagnol aliitumikia Bayern Munich katika michezo zaidi ya 180 huku akifanikiwa kubeba makombe 10 akiwa na klabu hiyo, ni wazi kwamba anaijua vyema Bayern na anajua utamaduni wa klabu hiyo.

Mwaka 2008 Sagnol aliingia katika vichwa vya habari nchini Ujerumani baada ya ugomvi mkubwa kati yake na kocha wa Bayern Munich kipindi hicho Ottmar Hitzfield ugomvi uliopelekea Sagnol kutoswa katika kikosi cha Bayern kilichosafiri kwenda kucheza na St Petersburg.

Mwaka 2000 mchezaji huyo aliingia katika mzozo na klabu ya Ufaransa ya Monaco kuhusu maslahi baada ya Sagnol kudai ya kwamba Monaco walikuwa wakimlipa kiasi kidogo sana cha pesa na kumuona mjinga kwa kuwa alikuwa na umri mdogo kitu kilichomfanya kuachana nao.

Sagnol ambaye kwa mashabiki wa Bayern anafahamika kama “The God Of Cross” aliwahi kuifundisha klabu ya Ligue 1 ya Bordeaux lakini pia amewahi kuifundisha timu ya taifa ya Ufaransa chini ya miaka 21 na baada ya uwepo wake katila benchi la ufundi la Bayern Munich sasa anakwenda kuwa kocha mkuu.

Mwanafunzi wa darasa la tatu apewa ujauzito, Kilombero
Aguero apata ajali ya gari