Mwanafunzi wa darasa la tatu mwenye umri wa miaka 13 katika shule ya msingi Makutano, katika kitongoji cha Igole wilayani Kilombero amekatizwa masomo yake kwa kufukuzwa shule baada ya kupewa ujauzito huku mtuhumiwa wa tukio hilo Samuel Daudi akitoroka kwenda kusikojulikana.
 
Wazazi wa binti huyo ambaye hutembea kilometa nyingi kwenda shule, wakisema hawakugundua mapema kama kwa umri wake binti yao angeweza kubebeshwa ujauzito.
 
Suala la mimba za utotoni kwa wanafunzi wakiwemo wa shule za msingi wilayani Kilombero inadaiwa kuchangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo vishawishi na kurubuniwa kwa wasichana wadogo kutokana na umbali wa shule hizo na makazi ya watu.
 
Fabian Undole, ambaye ni Mwalimu mkuu wa shule hiyo, amesema wamekuwa na taratibu za kuwapima afya wanafunzi wa kike shuleni hapo kila baada ya miezi mitatu na kwamba jamii ya wafugaji imekuwa ikiongoza kwa matatizo hayo.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, Denis Londo amekiri changamoto kama hizo kujitokeza katika baadhi ya maeneo ingawa wameendelea kuchukua hatua kali na sasa wanaongeza nguvu kudhibiti kabisa tatizo hilo.
Video: INAUMA SANA! Binti mwenye ugonjwa wa ajabu asimulia mazito, apaza sauti kuokoa maisha yake

HRW yaitaka dunia kulaani ukandamizaji Rwanda
Huyu ndiye kocha wa muda aliyechukua nafasi ya Carlo Ancelotti