Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amefikisha kilio cha Wajasiriamali wanaojishughulisha na uzalishaji na uchakataji wa malighafi za Kilimo kwa Shirika la Viwango Nchini -TBS, wakilalamikia usumbufu wa kupata alama ya utambuzi wa bidhaa (Barcode).

Wajasiriamali hao, wamemueleza Mkuu huyo wa Wilaya kuwa, wanakumbana na usumbufu huo wa TBS kitu ambacho huwafanya kushindwa kufanya biashara na kupelekea bidhaa hizo kutotambulika na kukuza thamani ya ubora wa bidhaa zao.

Akizungumza kwenye semina maalumu ya mafunzo ya umuhimu wa nembo ya ubora wabidhaa zinazotolewa na TBS, Malisa amelishauri shirika hilo la Viwango Nchini, kufuatilia kero hiyo kwa ukaribu ili mjasiriamali apate alama hiyo ya utambuzi wa bidhaa.

Amesema, pindi TBS inapothibitisha bidhaa zoezi hilo liambatane na upewaji wa alama ya utambuzi, ili kuwaondolea usumbufu Wajasiriamali na Wafanyabiashara ambao hukosa kigezo hicho muhimu.

Robertinho akalia kuti kavu Simba SC
Gamondi afichua alipoishika Simba SC