Serikali imesema kuwa kampuni ya madini ya Barrick imekubali masharti yote na sheria mpya ya madini na kulipa dola za marekani milioni 300 sawa na shilingi bilioni 660 za kitanzania kama namna ya kuonesha uaminifu.
Hayo yamesemwa leo Ikulu jijini Dar es salaam, na waziri wa sheria na katiba Prof.Palamagamba Kibudi, wakati akitoa mrejesho wa kamati maalumu iliyoundwa na Rais JPM, kwa ajili ya kufanya majadiliano na wawakilishi kutoka kampuni ya Barrick.
-
Jela miaka Saba kwa kesi ya Wizi
-
Ujumbe mzito alioandika Zitto Kabwe kwa Tundu Lissu
-
LIVE BREAKING: Rais Magufuli apokea ripoti mazungumzo ya Serikali na Barrick
Amesema kuwa kampuini ya Barrick itaingia ubia na serikali ya Tanzania kwa asilimia hamsini kwa mhamsini katika biashara ya madini na kukubali kuwa serikali kuwa na asilimia 16 ya migodi yote ya Barrick.
Aidha amesema kuwa Barrick imekubali kujenga maabara na viwanda vya kuchakata makinikia nchini na kuachana na wafanyakazi wa mikataba na kuajili wazawa.
Mwenyekiti mtendaji wa Barrick John Thonton, amesema kuwa makubalianao haya yataenda kuidhinishwa na Bodi nchini Uingereza ambayo ina hisa asilimia 64.
Kupitia ukurasa wa Facebook Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameibuka na kukosoa makubalianao hayo ameandika hivi
“Linex Sunday Mjeda alipata kuimba kwa Kiha, Langa kutulila Mazuyabhu, maana yake mwehu anapochoma nyumba yake ili aote moto, naona mmepata noah wananchi wenzangu, Narudia kuongoza ni maarifa si mabavu, bila aibu watatokea watu watatetea hili agizo la Tanzania na Barrick, Hivi $300 ni % ngapi ya $194?” ameuliza Zitto Kabwe.