Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe ameomba muongozo wa Spika kuhusu hali ya usalama wa nchi, kwa kuwa matukio ambayo yanaendelea kutokea ya kihalifu yamekosa hitimisho Lake.

Amesema hayo wakati akiomba muongozo ndani ya bunge kwa kumtaka Spika wa bunge, Job Ndugai kukubali ombi la kamati ya usalama ya bunge kukutana na vyombo vya usalama ili yaweze kupatikana majibu ya matukio yanayoendelea kutokea.

“Mhe. Spika katika taifa letu katika kipindi cha muda mrefu kumekuwa yakitokea matukio mbalimbali ambayo sisi kama wawakilishi wa wananchi tuna wajibu wa kupata taarifa sahihi juu ya muendelezo wa matukio hayo ambayo hayana hitimisho,”amesema Bashe

Hata hivyo, kwa upande wake Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Job Ndugai amekubali hoja iliyotolewa na mbunge huyo na kutoa amri kwa kamati ya ulinzi na usalama ya bunge ikutane ili waweze kupanga jinsi ya kulishughulikia jambo hilo.

 

 

Video: Mbappe aanza kuonyesha cheche zake PSG
Video: Tundu Lissu dunia nzima, Vigogo waanza kukamatwa