Katibu mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally ametoa ushauri wa vijana kuwa wabunifu kwa sababu bila kuchapa kazi maisha yataendelea kuwabana kwani kuwa na shahada ya chuo kikuu hakumaanishi kupata fedha kirahisi bila ya kuwa na maarifa.
Amesema yeye binafsi ana historia ndefu kabla ya kuwa katibu mkuu wa CCM kwakuwa alipokuwa anasoma na baada ya kuhitimu masomo alifanya kazi ya uchuuzi kwenye magulio mbalimbali wilayani Bukoba.
Bashiru ameyasema hayo jana alipokuwa akitoa salamu za CCM katika kata ya Mayondwe wilayani Muleba kwenye shughuli ya dua ya kuombea amani ya nchi.
Tanga wapewa DK. 30 kusherehekea mwaka mpya
“Vijana bila kufanya kazi maisha yatabana na vyuma vitabana kwelikweli. mimi ni katibu mkuu kwa sasa lakini hakuna gulio nisilo lifahamu hapa Bukoba na muleba kiasi ” amekazia Bashiru.
Na kuonya kuwa mtu akiwa na elimu ya shahada kichwani asifikiri kuwa ndio amepata fedha bali maarifa aliyoyapata ndiyo yatakayotengeneza mafanikio yake.
Hata hivyo amesema CCM ina jukumu la kutunga sera wezeshi ili kundi kubwa la vijana liweze kupata mazingira mazuri ya fursa mbalimbali zikiwemo za biashara, kilimo na viwanda.