Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 5 kwa Waziri wa maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na katibu mkuu wa wizara hiyo, Prof. Adof Mkenda waondoe tofauti zao vinginevyo atatengua uteuzi wao.

Magufuli ametoa agizo hilo leo Desemba 31, 2019 alipokuwa akizungumza na maafisa na askari wanyamapori na Hifadhi ya misitu wa hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo ambako ametembelea na kujionea vivutio vya utalii.

“Nafahamu watendaji wenu wa juu, katibu mkuu na waziri kila siku wanagombana na ninawatazama taratibu, nilishampa kazi katibu mkuu kiongozi awaite awaelezee lakini wasipobadilika nitawaondoa” amesema Magufuli.

Na kuongeza kuwa ” siwezi kuwa na watendaji wa kuwateua mimi halafu kila siku wanagombana, kuna mambo mengi hayaendi, katibu hamheshimu waziri na waziri nae hataki kwenda na katibu mkuu, siwezi kuvumilia hilo.

Aidha Rais Magufuli ameiongezea muda Bodi ya TANAPA iliyomaliza muda wake chini ya mwenyekiti Jenerali mstafu, George Waitara kutokana na kuridhishwa na kazi nzuri walizofanya chini ya uongozi huo ikiwemo kuunda Jeshi usu la Askari wanyama pori na hifadhi ya misitu.

Video: Nugaz amrarua Shaffih Dauda bila woga: ''Wewe ni nani Tanzania hii"
Bashiru afunguka alivyouza gulioni " Shahada ya chuo haimaanishi kupata fedha"