Basi la Tashrif lililokuwa likitoka Tanga kuelekea Dar es salaam, limeungua moto na kuteketea maeneo ya Pongwe karibu na mizani.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo wakati akizungumza na Dar24, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Benedict Michael Wakuyamba amesema ajali hiyo imetokea leo Septemba 26, 2017 ambapo basi hilo lenye namba za usajili T T361 DCF limewaka moto katika eneo la Pongwe jiji Tanga, na hakuna madhara yoyote kwa binadamu zaidi ni hasara ya mizigo ilikuwa imewekwa kwenye buti.

Amesema kuwa basi hilo liliokuwa likiendeshwa na dereva, Hemedi Ali (35) mkazi wa Tanga lilikuwa likitokea Tanga kuelekea jijini Dar es salaam lilikuwa limebeba abiria 26 lilipofika eneo hilo liliwaka moto.

Kamanda Benedict amesema kwamujibu maelezo ya awali ya Dereva huyo anadai alianza kuona cheche za moto kwa chini upande wa tairi ya gari ndipo aliposimamisha gari hilo na kuwataarifu abiria kushuka ndani ya basi hilo.

Amesema wakati abiria waliposhuka basi hilo lilipuka moto na kuungua hadi kuteketea.

Aidha, amesema kuwa bado chanzo cha moto huo hakijajulikana hivyo jeshi hilo linafanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.

Mipango ya timu za taifa za vijana
Mwigulu awatumia salamu ‘watu wasiojulikana’, akataa ya Chadema