Takriban watu 41 wamefariki baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuanguka kwenye korongo na kuwaka moto kusini-magharibi nchini Pakistan hii leo Januari 29, 2023.
Katika tukio la kwanza, ajali hiyo ya basi ilitokea karibu na mji wa kusini wa Bela, uliopo katika Mkoa wa Balochistan, ilipokuwa ikisafiri kuelekea mji wa bandari wa Karachi ambapo Afisa wa eneo hilo Hamza Anjum alisema miili 40 ilipatikana na watu wawili walijeruhiwa.
Wakati hilo likitokea, eneo la kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo watoto wasiopungua 10 wenye umri wa kati ya miaka saba na 14 wamekufa maji katika ajali ya boti.
Amesema, manusura wawili waliosalia walikuwa katika hali mbayana na inasemekana basi hilo liligonga nguzo kwenye daraja kabla ya kuporomoka kwenye korongo hilo kubwa.
Katika tukio la pili, watoto hao 10 wamekufa maji baada ya kutokea kwa ajali ya boti ziwa Tanda, lililopo karibu na Kohat huko Khyber Pakhtunkhwa, Afghanistan ambapo Afisa wa eneo hilo Mir Rauf amesema watoto 11 waliokolewa, huku sita wakiwa katika hali mbaya na wengine tisa wanaaminika kupotea.
Rauf amesema kuwa boti waliyokuwa wakisafiria ilikuwa imebeba abiria mara mbili zaidi ya ya uwezo wake katika safari ya mchana kutoka madrasa ya eneo hilo shule ya Kiislamu kabla ya kupinduka.