David Beckham amepigwa marufuku kuendesha gari kwa miezi sita kwa kosa la kutumia simu wakati akiendesha gari.
Wakili wa Beckham, Gerrard Tyrrell amesema mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United ” haikumbuki siku hiyo au tukio hilo hivyo hakuna utetezi wa kilichotokea.
Raia mmoja nchini humu alifanikiwa kumpiga picha wakati akiendesha gari yake aina ya Bentley akiwa foleni na kuiambia mahakama ambapo muendesha mashtaka amelalamika na kusema badala ya kutazama mbele na kuangalia barabara alionekana akitazama mapajani mwake.
Jaji katika mahakama hiyo aliongezea kuwa hata kama kasi ya gari ilikuwa taratibu kwenye foleni ‘hakuna kisingizio’ chini ya sheria.
Beckham, mwenye umri wa miaka 44, ametozwa faini ya £750 sawa na Milioni 1.9 kwa pesa ya Kitanzania, pia ameagizwa alipe £100 sawa na Shilingi 250,000 kwa pesa ya kitanzania na gharama ya kesi na malipo ya ziada ya £75 sawa na shiilingi 193,000 kwa pesa ya kitanzania katika siku saba zijazo.
Tyrrell ameiambia mahakama kwamba Beckham hufurahia kuendesha gari.
“Huwapeleka watoto shuleni kila siku na mara nyingine hurudi kuwachukua anapoweza, na kuwanyima hilo ni jambo ambalo hana budi kulikubali,” amesema
Ni kinyume cha sheria nchini Uingereza kushika simu wakati unaendesha gari. Mtu anaweza kuadhibiwa kwa kupunguziwa pointi kwenye leseni na kutozwa faini ya £200 – lakini kutokana na uzito wa makosa unaweza kufikishwa mahakamani na ukahukumiwa adhabu kali zaidi.