Beki wa kushoto wa Uganda, Mustapha Kizza ameweka wazi kuwa yupo tayari kujiunga na Azam FC kama watakubaliana naye kila kitu kwani matarajio yake kuona anakipiga katika Ligi ya Tanzania Bara.

Kiiza mwenye umri wa miaka 22 kwa sasa anakipiga katika Klabu ya Polisi Uganda huku akiwahi kucheza katika soka la kulipwa nchini Marekani katika klabu ya Montrel Impact.

Kizza amesema kuwa kama Azam FC watakuwa tayari kumsajili yeye yupo tayari kujiunga na miamba hiyo kutokana na ukubwa wa Azam FC kwa sasa na malengo yao waliyonayo haswa katika michuano ya kimataifa.

“Nimekuwa nikiwaona Azam FC kwa jinsi ambavyo wanatamani kufanya vyema katika michuano ya kimataifa, hivyo na mimi niwahakikishie kuwa watakuwa tayari kunisajili mimi nipo tayari kwa hilo.

“Azam FC naamini ni timu ambayo inanifaa kwa kuwa hata mpira wa Tanzania kwa sasa umekuwa ni mkubwa jambo ambalo linapelekea wachezaji wengi kutamani kucheza katika ligi yao ambayo naamini baada ya miaka mitano itakuwa ni ligi kubwa sana,” amesema beki huyo.

Hata hivyo Kiiza anahusishwa kuwaniwa na Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans ambao wamedhamiria kujiimarisha ili kuendelea kutamba katika Soka la ndani nan je ya Tanzania msimu ujao 2023/24.

Serikali yaibua fursa miradi ya kijamii, biashara ya kaboni
Jaji Mbarouk ataka weledi usimamizi wa Uchaguzi