Hakuna mchezaji mzuri anayenunuliwa kwa bei rahisi na hii imethibitishwa na Real Madrid baada ya kuonyesha jeuri ya fedha kufuatia usajili wao uliovunja rekodi England baada ya kumsajili kiungo, Jude Bellingham kutoka Borussia Dortmund.

Kiungo huyo wa kimataifa wa England sasa anaweka rekodi ya kuwa mwanasoka ghali zaidi wa Uingereza kufuatia uhamisho wake wa kutoka Dortmund kutua Santiago Bernabeu kugharimu Pauni 115 milioni.

Aidha mbali na Bellingham, mchezaji mwengine wa bei kubwa England ni Jack Grealishi wa Machester City.

Manchester City ilimnunua kiungo huyo kwa ada ya uhamisho wa Pauni 100 milioni akitokea Aston Villa, katika usajili wa dirisha la kiangazi.

Ingawa alichukua muda mrefu kufiti kikosini msimu wake wa kwanza, sasa kiungo huyo amekuwa mchezaji mwenye mchango mkubwa.

Msimu uliopita alicheza mechi 50 na akasaidia Man City kubeba mataji matatu na kufidia pesa aliyonunuliwa. Grealish alikuwa gumzo mtandaoni kutokana na shangwe lake ubingwa kwa muda wa siku nne.

Mchezaji mwingine wa bei ni beki wa kati wa Machester United, Harry Maguire, beki huyu alijiunga na Manchester United tangu mwaka 2019 kwa kitita cha Pauni 85 milioni akitokea Leicester City.

Maguire amechezea Man United mechi 157, lakini amepitia kipindi kigumu. Beki huyu hakutoboa chini ya kocha Erik ten Hag na taarifa zinaripoti huenda akaondoka kutokana na kutopewa muda wa mwingi wa kucheza.

Sancho alisajiliwa na Manchester United akitokea Borussia Dortmund mashabiki walikuwa na matarajio makubwa kutoka kwake. Kama ilivyokuwa Maguire, winga huyu hakuwa na misimu mizuri.

Hata hivyo kocha Erik ten Hag bado anaamini staa wake huyo ana kipaji cha kucheza soka. Msimu wake wa kwanza Sancho alifunga mabao nane katika mechi 38 alizocheza.

Kiwango chake kilishuka kutokana majeraha na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.

White alijiunga na Arsenal mwaka 2021 kwa ada ya ujamisho wa Pauni 50 milioni akitokea Brighton.

Ingawa mashabiki waliponda kiwango cha pesa aliyonunuliwa, lakini beki huyo amekuwa tegemeo kikosini kinahonolewa na Mikel Arteta.

Winga huyo wa zamani wa Liverpool alijiunga na Mancheter City kwa Pauni 49 milioni mwaka 2015. Alifunga mabao 131 katika mechi 339 alizocheza Etihad kabla ya kutimkia Chelsea.

Msimu uliopita alicheza mechi 38 katika mashindano yote akiwa na uzi wa Chelsea.

Charles Lukula kuibukia The Crested
Ukubwa wa bajeti utumike kufanya tafiti za Kilimo - Malisa