Imefahamika kuwa Kocha Mkuu mpya wa Simba SC Abdelhak Benchikha anatarajiwa kutua nchini muda wowote kuanzia leo Jumatatu (Novemba 27), huku akishuka na makocha wawili katika kikosi hicho.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu kocha huyo atangazwe kumrithi Kocha kutoka nchini Brazil Robert Olivier ‘Robertinho’ aliyesitishiwa mkataba wake hivi karibuni.

Robertinho amesitishiwa mkataba ikiwa saa chache tangu mu hiyo, itoke kufungwa mabao 5-1 katika mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Young Africans.

Taarifa zinaelezwa kuwa kocha huyo anatarajiwa kutua nchini akiwa na kocha msaidizi na viungo.

Mtoa taarifa huyo amesema kuwa upo uwezekano mkubwa wa kocha huyo, kukaa benchi kuingoza timu hiyo, katika mchezo wa pili wa Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana mwishoni mwa juma hili.

Ameongeza kuwa wakati makocha wakitarajiwa kuungana na timu hiyo, kocha, Selemani Matola ana nafasi kubwa ya kusalia kwenye benchi la ufundi.

“Kuanzia leo Jumatatu, kocha Benchikha atatua nchini pamoja na makocha wawili wa Makipa na Viungo kwa ajili ya kuimarisha kikosi chetu.

“Mara baada ya kutua nchini moja kwa moja ataanza programu ya kukinoa kikosi chetu, ambacho kimetoka kupata matokeo mabaya katika Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa.

“Benchikha huenda akaongezewa Matola katika sehemu ya benchi lake la ufundi” amesema mtoa taarifa huyo.

Akizungumzia hilo Meneja wa Habari na Mawasilinao, Ahmed Ally alisema kuwa “Haraka kocha wetu atawasili nchini kwa ajili ya kuanza kibarua cha kukinoa kikosi chetu, kikubwa mashabiki wawe wavumilivu katika kipindi hichi ambacho timu inapitia.

Madereva warudishwa Darasani Hanang'
Aaron Ramsdale amfurahisha Kocha Arsenal