Jeshi la Polisi Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara, limefanya ukaguzi wa vyeti kwa Madereva wa Daladala na Mabasi ya abiria, ili kuwabaini wasiokuwa na sifa ya kufanya kazi hiyo.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo Stendi Kuu ya mabasi Kateshi, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilayani humo Mkaguzi wa Polisi, Volca Willa amesema uhakiki huo utahakikisha madereva wote wa abiria wanapata mafunzo katika vyuo vya udereva vinavyotambulika na serikali.

Amesema, Dereva aliyepata mafunzo na kufaulu huwa mtumiaji nzuri wa barabara kwani ataendesha kwa kuzingatia Sheria na kanuni za usalama barabarani na pia tayari wameanzisha Operesheni ya kukagua vyeti kwa madereva wa daladala na magari makubwa ya abiria.

Aidha, amesema zoezi hilo linalenga kuhamasisha madereva kwenda shule na kuzuia ajali za barabarani, ambapo jumla ya Madereva 89 na vyeti 120 vimehakikiwa na zoezi hilo litaendelea mpaka mwishoni mwa mwaka 2023.

Wolves kumng'oa Aaron Ramsdale Arsenal
Benchikha kutua na wasaidi wake Simba SC