Taasisi kubwa za kifedha Duniani zinawekeza kwenye makampuni yanayotengeneza Dawa za Jadi za Kichina zinazodaiwa kuwa na viungo vya chui na Kakakuona.
kwa mujibu wa Ripoti ya Mamlaka ya Uchunguzi wa Mazingira – EIA, inaonyesha kuwa benki 62 na taasisi za fedha zimefungamanishwa na vikundi vitatu vya dawa vinavyotengeneza bidhaa tisa zenye madai ya viungo vya chui au kakakuona.
Miongoni mwa Makampuni yanayotajwa ni pamoja na majina makubwa ya huduma za kifedha ya Uingereza ya HSBC, Prudential na Legal & General na makampuni ya uwekezaji ya kimataifa kama Goldman Sachs, UBS, Deutsche Bank, na BlackRock.
Wanyama hao, pia wamo kwenye orodha ya Mkataba wa Biashara ya Kimataifa ya Wanyama na Mimea Walio Hatarini Kutoweka (CITES) inapiga marufuku biashara ya kimataifa inayohusiana nao, kwa lengo la kuhifadhi spishi hizo.
Kampuni tatu za dawa zilizochunguzwa na EIA ni kikundi cha Tong Ren Tang, kikundi cha Dawa cha Tianjin, na Kikundi cha Dawa cha Jilin Aodong.
Ni muhimu kutambua kuwa si kampuni zote zilizotajwa katika ripoti ya EIA zinafanya uwekezaji katika kila kampuni hizi tatu, lakini zote zimehusika kwa namna moja au nyingine.
Kwenye tiba ya jadi ya Kichina (TCM), mfupa wa chui hutumiwa kama mbadala wa mfupa wa simba. Mfupa wa simba unasadikiwa kuimarisha mifupa na mishipa ya binadamu, na kupunguza maumivu.
Magamba ya pangolin yanadaiwa kusaidia mzunguko wa damu, mchakato wa kunyonyesha, na kupunguza maumivu. Hata hivyo, madai haya hayathibitishwi kisayansi.