Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Izack Njenga amewataka Wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania kuongeza wigo kiutendaji, kitu ambacho kitafungua fursa nyingi hasa za mazao ya biashara na kuongeza kipato kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kiujumla, huku akisisitiza kuwa kitendo hicho kina maana kubwa.

Balozi Njenga ametoa wito huo wakati akifanya mahojiano maalum na Dar24 Media hivi karibuni na kusema uongezaji wa wigo wa ufanyaji wa biashara utapelekea hata bei za mazao kuongezeka na hivyo Wakulima kuongeza pato lao kwani bei itapaa.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Izack Njenga.

“Mkulima wa mpunga kule Mbeya anaweza kuwa hajafika Kenya, lakini mpunga aliolima ukawa unaliwa kwa wingi kule, na hii maana yake ni kwamba kama unaliwa kule basi unauzika hivyo biashara inapozidi kutanuka ndivyo na kipato huongezeka ni lazima tushirikiane na biashara zisonge mbele,” amesema Balozi Njenga.

Aidha ameongeza kuwa, biashara kati ya Tanzania na Kenya ina maana pana kwakua italeta muunganiko wa mambo mengi na kupelekea watu kuinuka kiuchumi na kukidhi mahitaji yao ya kila siku, huku akisisitiza mamlaka za pande zote mbili kuweka mazingira wezeshi ili kufanikisha jambo hilo.

Serikali yautambua mwaka mpya wa Kiislamu
DCEA yajipanga kupigania uchumi wa nchi