Klabu ya Biashara United Mara imeendelea kupata neema, kufuatia Uongozi wa Mgodi wa dhahabu wa North Mara Gold Mine, kusaini mkataba wa kuendelea kuidhamini klabu hiyo yenye maskani yake makuu mjini Musoma mkoani Mara.

Biashara United Mara ambayo bado haijatambua hatma yake kwenye michuano ya Kimataifa, imekua ikidhaminiwa na kampuni hiyo ya uchumbaji madini (Dhahabu), tangu msimu uliopita.

Mkataba uliosainiwa kati ya pande hizo mbili, una thamani ya zaidi ya shilingi milioni 300, ambao utadumu kwa miezi 9, sawa na msimu mzima wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Pamoja na udhamini huo, Uongozi wa North Mara Gold Mine umeahidi kutoa dola za MArekani 45,000/= (zaidi ya shilingi milioni 100) kwa ajili kuisaidia timu hiyo itakaposhiriki katika mechi za kimataifa.

Mkataba huo umesainiwa mbele ya Katibu Tawala mkoa wa Mara Albert Gabriel Msovela kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Ally Hapi ambaye amewataka wachezaji na benchi la ufundi kuhakikisha timu hiyo inamaliza ligi ikiwa katika nafasi 3 za juu.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Barrick North Gold Mine Apolinary Lyambiko amesema mgodi huo utaendelea kuwa karibu na timu hiyo ili kuendelea kuwa alama ya mkoa wa Mara sambamba na kuleta burudani ya kandanda mkoani hapa.

Mlima Kilimanjaro wapoteza barafu kwa asilimia 90
Taifa Stars Stars yawekwa hadharani