Kikosi cha Namungo FC kimewasili jijini Dar es salaam leo Jumatatu (Novemba Mosi) tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Mzunguuko wa tano.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa keshokutwa Jumatano (Novemba 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, kunzia saa moja usiku.

Namungo FC wamewasili majira ya mchana jijini humo wakitokea mkoani Lindi wakiwa na kikosi kamili, ambacho kinaaminiwa kitaweza kuiduwaza Simba SC ambayo msimu huu haijaanza vyema Mshike Mshike wa Ligi Kuu.

Namungo inayoshika nafasi ya nafasi ya kumi ikiwa na alama 5, itahitaji ushindi katika mchezo dhidi ya Smba SC ili kujiongezea alama zitakazowapeleka katika nafasi ya juu kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Nayo Simba SC inayoshika nafasi ya nne kwa kuwa na alama 8, itahitaji kuutumia mchezo huo kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika mchezo wao wa jana Jumapili (Oktoba 31), dhidi ya Coastal union uliomalizika kwa sare ya 0-0.

Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi, Simba SC iliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Nuno atemwa Tottenham Hospurs
Simba SC yanasa kwa Rulani Mokwena