Klabu ya Tottenham Hospurs imetangaza kuachana na Meneja kutoka nchini Ureno Nuno Herlander Simões Espírito Santo, kufuatia mambo kumuendea mrama tangu alipokabidhiwa jukumu la kuwa mkuu wa benchi la ufundi la klabu hiyo.

Nuno alikabidhiwa jukumu la kuwa meneja wa Spurs, Juni 30-2021, baada ya klabu hiyo kuachana na José Mourinho, ambaye nafasi yake ilishikwa kwa muda wa meneja kutoka nchini England Ryan Mason.

Taarifa kutoka Spurs ambayo iliothibitisha kuondolewa kwa Nuno imeeleza kuwa, pande hizo mbili zimekubaliana kuachana kwa wema na zimetakia kila la kheri.

Hata hivyo imeripotiwa kuwa, Uongozi wa Spurs umeshaanza mazungumzo na aliyewahi kuwa meneja wa Chelsea Antonio Conte ili achukue nafasi ya Nuno.

Kwa sasa Conte hana kazi, baada ya kuachana na Inter Milan mwishoni mwa msimu uliopita 2020/21.

Kabla ya kujiunga na Spurs Nuno alikua meneja wa kikosi cha Wolverhampton Wanderers, ambacho alikinoa na kukifanya kuwa kikosi tishio katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu ya England.

Taifa Stars Stars yawekwa hadharani
Namungo FC yawasili Dar, kukabili Simba SC jumatano