Mwandishi wa habari za michezo mwandamizi Edo Kumwembe amesema anaamini kiungo kutoka DR Congo Mukoko Tonombe hana muda mrefu, ndani ya kikosi cha Young Africans.

Kumwembe ambaye pia hufanya shughuli za uchambuzi wa soka la Bongo na lile la Kimataifa kupitia kituo cha Radio cha Wasafi FM, amesema kiungo huyo ana wakati mgumu wa kurudi kwenye kikosi cha kwanza cha Young Africans, ambacho kwa sasa kimejitosheleza katika nafasi ya Kiungo.

Akizungumza mapema leo Jumatatu (Novemba Mosi) kupitia kipindi cha Sports Arena cha Wasafi FM, Kumwembe amesema: “Nahisi safari ya Mukoko Tonombe imewadia. Atacheza wapi?”

“Pale katikati Aucho na Yanick Bangaala wanaonekana kuwa na uwezo mkubwa wa umiliki wa mpira kuliko Mukoko.”

“Huyu Mukoko ni mzuri wakati timu haina mpira lakini timu ikiwa na mpira hana umiliki mzuri wa mpira.”

“Kitakachomrudisha Mukoko uwanjani ni kama mlinzi mmoja wa kati ataumia au atakuwa na kadi zitakazomuweka nje ya uwanja. Kama Bakari Mwamunyeto au Dickson Job mmoja akiumia basi Bangala anaweza kurudi nyuma na Mukoko akacheza na Aucho.”

“Vingnevyo sioni nafasi ya Mukoko kikosini.”

Adhabu ya kadi nyekundu alioonyeshwa Mukoko wakati wa mchezo wa Fainali wa Kombe la Shirikisho 2020/21 dhidi ya Simba SC, huenda imekua sababu ya kupotea kwenye kikosi cha kwanza cha Young Africans, kwani msimu huu 2021/22 ulipoanza alikua akiitumikia adhabu hiyo.

Hatua hiyo ilimkosesha kiungo huyo kuwa sehemu ya kikosi cha Young Africans, na nafasi yake kuchukuliwa na viungo Khalid Aucho na Yanick Bangaala, na bado anaendelea kukaa benchi.

Simulizi: Penzi la Dada yangu wa Tumbo moja lilivyonisahaulisha kuoa
Nembo rasmi miaka 60 ya Uhuru Tanzania