Rais wa Marekani Joe Biden amelihutubia bunge la nchi hiyo kwa mara ya kwanza akiwa rais na kutumia sehemu ya hotuba yake kuwaonya washindani namba moja wa kibiashara wa hiyo amabo ni China.
Rais huyo amelieleza taifa lake kupitia hotuba hiyo ya bungeni kuwa katika mazungumzo yake na rais Xi Jinping wa Uchina, ameweka wazi msimamo wake kuwa japo Marekani haitafuti mgogoro na Uchina, lakini pia atalinda maslahi yake ya kibiashara kwa nguvu zake zote.
Biden amesema kuwa Marekani haitakaa kimya wakati makampuni ya kichina yakitia usalama wa makampuni ya kimarekakani na hata ajira za raia wake.
“Marekani itasimama kidete dhidi ya tabia zisizo za mizania katika biashara kutoka Uchina. Mambo ambayo yanawaminya wafanyakazi wa Marekani na viwanda vyao. Mambo hayo ni kama kutoa ruzuku kwa viwanda vinavyoeindeshwa na serikali, wizi wa teknolijia ya kimarekani paoja na hatimiliki .” amesema Rais Biden
Hata hivyo mahusiano baina ya Marekani na Uchina yapo katika kilele cha migogoro kwa sasa.