Kufuatia kuripotiwa kwa taarifa ya watu watatu ambao ni wafanyabiashara wa kuuza nyama (mishikaki) kukamatwa wakichinja mbwa maeneo ya Msamvu, Manispaa ya Morogoro kituo hiki kimemtafuta Kamanda wa Polisi ili kupata ukweli wa taarifa hiyo.

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Fotunatus Musilimu amekiri kushikiliwa kwa watu hao na kwamba uchaguzi unaendelea ili kubaini ukweli Kuwa mnyama huyo Kuwa ni mbwa.

Amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na idara ya wanyama wanafanya uchunguzi na baada ya uchunguzi kukamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Polepole: Wajumbe kutoka sehemu mbalimbali watashiriki
Biden aionya China