Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Pwani,  David Mramba ameapa kulivalia njuga suala la Mtendaji anayedaiwa kupokea Mil. 8 za kuziba barabara iliyoharibika, malalamiko yaliyowasilishwa na Katibu Siasa na Uenezi Kata Kibaha Vijijini, Pendo Ernest.

Mramba amesema hayo Mlandizi Wilayani Wibaha Mkoani Pwani, wakati akitoa mada kwa Makatibu wa Siasa, uenezi na mafunzo Kata ya Kibaha Vijijini na kusema fedha hizo hazilingani na kazi iliyofanyika.

“Tunajua kwamba pesa ilitolewa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini kiasi cha Mil.nane lakini kifusi kilichowekwa ni kidogo hivyo kimezalisha tope ambalo hata magari yanashindwa kupita kutokana na barabara kuzidi kuwa mbovu” amesema.

Katibu wa CCM Tawi la Mkwajuni Kata ya Mtambani Kibaha Vijijini Khadija Ameir Maguto alimueleza Mramba kuwa wananchi wake wanahitaji utekelezaji wa barabara ya Makofia Mzenga Bagamoyo.

“Sisi viongozi tunapata malalamiko mengi kutoka kwa wananchi zoezi la ujenzi limeanza miaka mingi lakini hakuna utekelezaji tuliambiwa kuwa Desemba mwaka 2023 tutalipwa lakini hadi sasa hakuna utekelezaji.”

TAWA yapokea Meli ya Watalii zaidi ya 200
Mauricio Pochettino azua kizungumkuti Chelsea