Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameridhia serikali kununua madini ya Tanzanite kwa mfanyabiashara wa madini katika migodi ya Madini ya Tanzanite Mirerani wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara bila ya kumpunja mchimbaji huyo mdogo hata shulingi moja.

Waziri wa Madini Dotto Biteko ameshuhudia halfa ya ununuzi wa vipande viwili vya madini hayo kwa bilionea Amselim Kavishe huku kimoja kikiwa na uzito wa kilo 1.477 na kingine kikiwa na kilo 3.747 vyote vikiwa na dhamani ya bilioni 2.2

Waziri Biteko amesema Rais Samia amekuwa akitoa muongozo unaoleta tija katika sekta ya madini na mikakati ya kukuza uzalishaji wa madini ya Tanzanite.

”Tunakuja na mfumo amabao utaifanya Tanzanite ifanyiwe biashara katika mazingira ambayo Mirerani itakuwa mnufauika wa kwanza kabla ya mtu mwingine na huo mfumo utakuwa wa wazi na mfumo shirikishi , utaratibu wa watu wawili kujifungia ndani na katunga kanununi tumeuhama” amesema Biteko.

Hii imekuwa mara pili kwa Tanzanite yenye uzito mkubwa ambapo kwa mara ya kwanza ilimtoa bilionea Saniniu Laizer mwaka 2020 naye bilionea Kavishe ameeleza kwamba sera bora za serikali ndio siri ya mafanikio yake.

Vifaa vya kupigia kura Kakamega vyawasili
Wimbi jipya la vurugu lauwa watu 12