Kikosi maalumu cha Polisi nchini Uganda Flying Squad kinachunguza wizi uliofanyika kwenye mashine za kutoa na kuweka pesa (ATMs) katika vitongoji vinne vya Jiji la Kampala na matokeo yake sh bilioni mbili zikapotea katika kipindi cha wiki mbili.
Mtandao wa wezi 15 ulikamatwa siku chache baada ya timu ya walinzi ya kampuni ya ulinzi ya SGA Security Group kutumwa kuongeza fedha kwenye mashine ya ATM ilyopo kwenye bank ya kitongoji cha Nansana ambako fedha zilipotea.
Maafisa wanaojaza fedha kwenye ATM walipewa fedha nywila na alama za siri ili kuchukua fedha atika ATM ya Nansana na walikuwa na ulinzi mkali.
Hata hivyo maofisa hao pamoja na walinzi wao kwa pamoja walitoweka jambo lilioifanya kampunzi ya SGA Security Group kufanya uchunguzi amabo ulibaini kuwa bilion 2 ziliibiwa huenda na wafanyakazi hao.
Timu ya maofisa wa usalama wa kampuni ya SGA ilisambazwa katika eneo la Nansana kwaajili ya kile kilichodhaniwa kuwa ni shughuli ya kawaida ya kuongeza fedha kwenye ATM ikiwa na wahudumu watano.
Hata hivyo ilibainika kuwa wafanyakazi hao wote walipotea na kiasi cha fedha ambacho hakifahamika.