Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na wakala wa Ufundi wa Umeme(TEMESA) wametakiwa kusimamia miradi ya barabara na kivuko kwa weledi mkubwa na ikamilike kwa muda uliopangwa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Godfrey Kasekenya wakati wa halfa ya utiaji saini wa mikataba ya ujenzi wa barabara ya Sengerema Nyehunge yenye urefu wa kilometa 54.4itakayogharimu zaidi ya sh bilioni 73.47 na ujenzi wa kivuko kitakachotoa huduma katika kivuko cha Buyangubalika Mkoni Mwanza.

“Barabara ya Sebgerema Nyehunge ni ya kimkakati na kiuchumi itakayojengwa kwa kiwango cha lami lengo kuwaondolea wananchi changamoto ya usafiri na kuwaboreshea mtandao wa barabara kwa kuongeza ufanisi kwa sekta ya usafirishaji”.

Aidha amesema utekelezaji wa mradi huo utatumia fedha za ndani ikiwa ni mikakati na juhudi za uboresha maisha ya wananchi wa Sengerema na ukikamilika utaimarisha shughuli za kiuchumi.

Kasekenya alisema mikoa iliyoko Kanda ya Ziwa ambayo ni Mara, Geita, mwanza na Kagera inaunganishwa na Ziwa kwa sehemu kubwa hivyo Rais Dkt. Samia ameamua kujenga vivuko vipya vitano katika mikoa hiyo kukuza uchumi.

Pia ameishukuru Serikali kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya miundombinu inayosimamiwa na Wizara ya Ujenzi na katika kuhakikisha Tanzania inaendelea na kuboresha miundombinu ya barabara reli, anga na usafir kwa njia ya maji.

Makala: Mzimu wa Kibwetere na mfungo tata wa kifo Kenya
Neno la shukurani kutoka Young Africans