Serikali imetoa takribani Shilingi Bilioni 21 kwa ajili ya kuboresha shule 85 za Kata hapa nchini ili ziwe na Kidato cha Tano na Sita hali itakayoongeza ubora wa kiwango cha elimu na kuimarishwa kwa miundombinu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Selemani Jafo amapo amesema kuwa dhamira ya Serikalini katika kuboresha sekta ya elimu ambapo kila mwezi imekuwa ikitoa takribani Bilioni 23 zinazotumika kugharimia elimu bure hali inayochochea kuongezeka kwa wanafunzi.
.“Tumejenga madarasa mengi na vyoo vingi ili kuendana na kasi ya udahili wa wanafunzi na pia tutahakikisha kuwa kuna kuwa na uwiano katika mgawanyo wa walimu katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Aidha, ameongeza kuwa Serikali katika kuboresha huduma za Afya imeshapeleka fedha katika vituo 172 kote nchini ili kuboresha huduma zinazotolewa na pia watumishi katika sekta hiyo wataajiriwa kwa kuzingatia mahitaji kutokana na nafasi zilizoachwa wazi baada ya zoezi la ukaguzi wa vyeti feki.
-
Rais Magufuli kuwatunuku wajumbe vyeti maalum
-
Video: Lulu akana kusababisha kifo cha Kanumba, Uteuzi wa Gavana mpya watikisa
-
Video: Daktari Muhimbili aeleza jinsi kope za bandia zinavyosababisha upofu
Hata hivyo, Jafo amewataka Viongozi wote katika Mikoa na Halmashauri kusimamia vizuri miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao ili thamani halisi ya fedha zilizowekezwa ionekane.