Mkurugenzi wa mafunzo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Benson Kigaila, ameendelea kusota rumande mpaka sasa huku dhamna yake ikiwa bado haijatolewa.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamanda Lazaro Mambosasa, amesema kuwa Kigaila yuko rumande katika kituo kikuu cha polisi kati, na kuongeza kuwa bado anashikiliwa mpaka pale uchunguzi utakapokamilika na kumpa dhamana, na hatimaye kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
“Kigaila bado tunaye dhamana yake bado hajapata, tunaendelea na uchunguzi tukijiridhisha tutampa dhamna na kumpeleka mahakamani kujibu mashtaka yake yanayomkabili,” amesema Mambosasa
Hata hivyo, Kigaila hapo jana alienda kuripoti kituoni kufuatia wito aliopewa na jeshi la polisi jijini Dar es salaam, na kuwekwa rumande mpaka sasa mbako yupo kutokana na tuhumza za kutoa uchochezi.