Mexico kwa mara ya pili sasa ndani ya mwezi mmoja imekumbwa na tetemeko kubwa la ardhi lililojeruhi na kuua watu wengi.
Kupitia tetemeko hilo, katika harakati za uokoaji imegundulika kuna binti mmoja ambaye amefunikwa na kifusi cha jengo la shule na yupo hai.
Hivyo waokoaji wanajaribu kumfikia msichana huyo mdogo aliyefukiwa na kifusi pindi tetemeko likitokea jana.
Waokoaji wamekuwa wakijaribu kumpitishia chakula na maji mtoto huyo akiwa ndani ya kifusi wakati taratibu za kumuokoa zikiendelea ili kufanya atoke salama katika hatari hiyo.
Kupitia tetemeko hilo watoto wapatao 21 walipoteza maisha baada ya jengo waliokuwamo kuvunjika huku wengine wakiwa bado ndani ya kifusi hicho.
-
Kitilya na wenzake watakiwa kuwa wapole
-
Polisi watumia Mabomu ya machozi kuwatawanya wakazi wa bonde la mto Msimbazi
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto amesema kuwa kila dakika imekuwa ikihesabika katika kuokoa maisha ya watu wake waliojeruhiwa na tetemeko hilo.
Aidha hadi sasa idadi kamili ya watu waliofariki dunia kutokana na tetemeko hilo ni watu 225.