Bodaboda kutumika kutoa elimu ya kujikinga homa kali inayotokana na virusi vya Corona watakaovaa vikoti maalumu vyenye maandishi ya kupinga maambukizo ya ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na waziri wa Afya Ummy Mwalimu kwenye ziara ya waziri mkuu Kassimu Majaliwa katika wilaya ya Hororo wilaya ya Mkinga.

Amesema kuwa Serikali imeamua kuja na kampeni hiyo baada ya kubainika kuna baadhi ya watu ya watu hawatumii mipaka kuingia nchini badala yake wanatumia njia za panya na bodaboda huwa wanawabeba.

”Serikali imeamua kuwatumia bodaboda kuwahamasisha watu wanaopitia njia za panya za mipakani kuwatengeneza vikoti maalimu vyenye ujumbe wa kuhamamsisha watu kupima na kuchukua tahadhari dhindi ya ugonjwa wa Corona” amesema

Kwa upande wake waziri mkuu ameelezaa kuwa watu wanaoingia nchini kupitia mipaka mablimbali wapimwe afya zao ili kujikinga na maambukizi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo homa inayosababishwa na virusi vya Corona.

Mwishoni mwa wiki waziri Ummy alipiga marufuku watu kukumbatiana kupigana mabusu na kushikana mikono katika kuchukua tahadhari ya kujikinga na homa hiyo.

Nchi za afrika zilizokumbwa na homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vipya jamii ya Corona zikiwemo Algeria ,Nigeria na Misri.

GUINEA-BISSAU: Rais wa mpito ajiuzulu baada ya siku tatu
Video: Unyanyapaa unavyochochea maambukizi ya ukimwi