Aliyetawazwa kuwa Rais wa Mpito wa Guinea-Bissau, Cipriano Cassama, amejiuzulu baada ya kukaa madarakani kwa siku moja akidai maisha yake na ya familia yake yapo hatarini.

Cassama alichaguliwa kama rais wa Mpito baada ya Chama cha PAIGC ambacho kina Wabunge wengi zaidi Bungeni kupinga matokeo ya Uchaguzi uliofanyika Desemba 2019 ambapo Umaro Cissoko Embalo aliapishwa kuwa rais.

Amesema amepokea vitisho vya kifo na anaona usalama wake upo hatarini hivyo anajiuzulu ili kuepusha mapigano katika Taifa hilo ambalo limekutwa na matukio tisa ya mapinduzi tangu mwaka 1980.

Baada ya Uchaguzi uliofanyika mwaka 2019, Rais aliyemaliza muda wake, Jose Mario Vaz alikabidhi madaraka yote kwa Embalo katika hoteli moja Jijini Bissau.

Cassama amesema mgogoro uliopo kati ya Umaro Sissoco Embalo na mpinzani wake Domingos Simões Pereira unapaswa kutatuliwa ili mshindi halali ajulikane.

Vijana wa " Ile pesa tuma kwenye namba hii" wakamatwa Mbeya
Bodaboda kutumika kutoa elimu ya Corona