Waziri wa nishati Dkt. Medard Kalemani ameitaka bodi mpya ya wakurugenzi wa shirika la umeme nchini (TANESCO) kusimamia shughuli zao kwa nidhamu na kufanya kazi kwa weledi ili kuboresha huduma za shirika hilo hapa nchini.
Dkt. Kalemani ametoa wito huo jijini Dodoma Novemba 13, 2019 wakati akitangaza majina ya wajumbe wapya wanane wa bodi ya wakurugenzi wa TANESCO ambao majukumu yao yameanza.
Wakulima Mtwara wauawa na watu wasiojulikana
Amesema baada ya kuwatangaza majina ya wajumbe hao akiwemo balozi Dkt. James Mwasi, Dkt. John Kihamba, John Kilwa na Dkt. Lugano Wilson Waziri huyo amewasisitiza kuzingatia nidhamu ya kazi ili kuweza kuleta mapinduzi chanya ya sekta hiyo.
“Simamieni majukumu yenu ipasavyo ili kuweza kufanikisha suala la huduma kwa shirika na hatimaye kuleta mapinduzi ya mwanga na mambo hayo yatafanikiwa ikiwa tutajituma na kusimamia kwa weledi majukumu yote ya shirika,” amefafanua Dkt. Kalemani.
Bunge lapitisha wanaoambukizwa Ukimwi kulipwa fidia
Hata hivyo katika upande mwingine Dkt. kalemani ameiagiza bodi hiyo mpya ya wakurugenzi kwenda kutatua kero za wateja na kuhakikisha tatizo la usambazaji wa umeme hapa nchini linamalizika na huduma kutolewa kwa wakati.
Kwa upande wake mwenyekiti mpya wa bodi ya wakurugenzi Dkt. Alexander Lugatona amesema shirika hilo la umeme TANASECO lina miradi mingi ya kimkakati inayolenga kuboresha huduma hapa nchini pamoja na kueleza changamoto zilizopo katika shirika hilo la umeme ikiwemo kuzidai baadhi ya taasisi za serikali zenye madeni.
“TANASECO ina miradi mingi na mipango ya kimkakati inayolenga kuboresha huduma zake hapa nchini licha ya uwepo wa changamoto mbalimbali ikiwemo kuzidai baadhi ya taasisi zenye madeni,” amefafanua Dkt. Lugatona
November 19, 2019 Rais John Pombe Magufuli alimteua Dkt. Alexander Lugatano kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la umeme Tanzania TANESCO.