Sakata la Ndege ya Serikali aina ya Bombadier iliyokamatwa nchini Canada limemlaza rumande Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS, Tundu Lissu.
Lissu anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam na amelazwa rumande ikiwa ni siku chache tangu alipoibua sakata la ndege ya serikali kukamatwa huko nchini Canada.
Aidha, katika mkutano wake na waandishi wa habari Lissu alisema kuwa ndege hiyo aina ya Bombadier imekamatwa nchini Canada na Kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd ya Montreal nchini humo na imeishtaki serikali ikipinga kuvunjiwa mkataba wa ujenzi wa Barabara ya Wazo Hill mpaka Bagamoyo.
-
Lissu akamatwa na Jeshi la Polisi Dar
-
Heche awazodoa wasomi, asema uzalendo si kuiunga mkono Serikali
Hata hivyo, hatua hiyo ya Mwanasheria huyo ilipelekea Serikali kukiri kuwa kuna mgogoro ambao umetengezwa na wanasiasa hao kwaajili ya kutaka kuikwamisha serikali kukamilisha manunuzi ya ndege hiyo.