Elimu bure inayotolewa Sera kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini, imeigusa Serikali ya Uingereza hivyo imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari  Jijini Dar es Salaam, kuhusiana na ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza.

Mahiga amesema kuwa Uingereza ni ya pili miongoni mwa Wahisani wanaotoa misaada ya kimaendeleo ikiifuatia Benki ya Dunia (WB), hivyo katika mantiki ya nchi zinazotoa misaada ya kimaendeleo kwa Serikali ya Tanzania ni ya kwanza.

“Serikali ya Uingereza ni moja ya nchi inayoongoza kwa uwekezaji nchini katika biashara, viwanda na  sekta binafsi. Pamoja na kuwa zipo nchi nyingi zaidi tunazoshirikiana nazo kibiashara,” amesema Balozi Mahiga.

Aidha, ameongeza kuwa mbali na ushirikiano uliopo baina ya Serikali za nchi hizo mbili, Uingereza imeendelea kushirikiana na baadhi ya Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NGO’s), Sekta ya Afya, Elimu na mahusiano baina ya watu na watu.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anyeshughulikia Masuala ya Afrika, Jumuiya ya Madola na Idara ya Ushirikiano katika Maendeleo ya Kimataifa, Rory Stewart amesema kuwa amefurahi kuja Tanzania na kupata fursa ya kutembelea baadhi ya shule Jijini Dar es Salaam na pia amefurahia Sera ya Elimu bure inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Mgufuli.

.

Bombadier yamkaanga Lissu, alala rumande
Magazeti ya Tanzania leo Agosti 23, 2017