Mshambuliaji kutoka nchini Ivory Coast Wilfried Bony amefanikiwa kuitumikia Swansea City kwa dakika 90 kwa mara ya kwanza tangu aliporejea klabuni hapo, akiwa na kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 23 usiku wa kuamkia leo.
Kikosi cha vijana cha Swansea City kilicheza dhidi ya vijana wa Derby County.
Kwa mara ya kwanza Bony alionekana akiwa na Swansea City mwishoni mwa juma lililopita katika mchezo wa ligi ya nchini England, ambapo walipoteza kwa kufungwa bao moja kwa sifuri dhidi ya Newcastle United.
Mshambuliaji huyo aliesajiliwa tena klabuni hapo akitokea Man city, alicheza mchezo huo akitokea benchi, na alionekana kutokua na kishindo cha kumili mikiki mikiki ya timu pinzani, hali amabyo ilitafsriwa hakuwa na utimamu wa mwili, hivyo alilazimika kutumika kwenye mchezo wa vijana chini ya umri wa miaka 23 usiku wa kuamkia leo.
Katika mchezo huo wa timu za vijana, Bony alifanikiwa kufunga bao la ushindi dakika ya 63.
Bonny aliuzwa kwa mkopo msimu uliopita kwenye klabu ya Stoke City, na mwezi julai alirejea Etihad Stadium, lakini meneja Pep Guardiola bado akaonyesha kutokua na mpango wa kumtumia msimu huu, hali ambayo ilimpa msukumo wa kumuuza Swansea City.