Mmiliki wa Klabu ya Chelsea Todd Bochly amekiri kufanya kosa kumfukuza kazi aliyekuwa Meneja wa kikosi cha klabu hiyo Thomas Tuchel, Septemba mwaka jana.

Inaelezwa kwamba uongozi wa Chelsea uliamini Graham Potter aliyechukua mikoba ya Tuchel angefanya vizuri katika michezo ya Ligi Kuu ya England, lakini matokeo yake mambo yalikuwa tofauti.

Tuchel alifukuzwa kazi kutokana na kutoelewana na mabosi katika masuala mbalimbali yaliyohusu maendeleo ya klabu.

Lakini baada ya Tuchel kutimuliwa, Chelsea ilimteua kocha wa zamani wa Brighton, Potter na kumpa mkataba wa miaka mitano, ila sasa wanajutia uamuzi huo.

Kwa mujibu wa Daily Mail, uongozi wa The Blues pamoja na mmiliki huyo wametambua kwamba walifanya kosa kubwa.

Ingawa ilielezwa Tuchel hakuwa mtu sahihi wa kuiona timu hiyo, kwa sasa mabosi wanaamini alistahili kupewa muda hadi mwisho wa msimu.

Kwa upande wa Potter, Chelsea imetambua ilitoa kiasi kikubwa cha pesa ilipomsainisha mkataba baada ya kuilipa Brighton ada ya Pauni 21.5 milioni.

Licha ya Potter kudumu muda mfupi, sasa wanaamini ana ubora na angepata mafanikio siku za usoni.

Kwa sasa Chelsea ipo mbioni kumnasa kocha wa zamani wa Tottenham, Mauricio Pochettino kwa makataba wa miaka mitatu. Pochettino alikuwa na mazungumzo na uongozi wa Chelsea  na mwishoni mwa juma lililopita pande hizo mbili zimefikia makubaliano ya awali.

Haaland aipa kazi ya ziada kampuni ya Nike
Wahukumiwa kunyongwa kwa kuiba chaja ya simu, kandambili