Michuano ya kombe la Dunia inaendelea leo ambapo timu ya taifa ya Nigeria ianatarajia kushuka dimbani leo kupambana na Iceland katika mchezo wao wa pili wa kundi ‘D’ huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa kwanza ambapo walifungwa na Croatia mabao 2-0.

Mchezo wa leo ni muhimu sana kwa Nigeria kwani wakipoteza mchezo huo watakuwa hawana tena matumaini ya kufuzu kucheza hatua ya 16 bora.

Katika kundi D Nigeria ndio wanashika mkia wakiwa hawajapata pointi yoyote huku Croatia wakiongoza kwa pointi 6 baada ya kushinda michezo miwili na Argentina wakiongozwa na nyota Lionel Messi wao pia wana pointi moja.

Wababe wengine watakaoshuka dimbani leo katika kundi ‘E’ ni Brazili ambao katika mchezo wao wa kwanza walishangazwa na Uswis kwa kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na leo wapo tena kibaruani kupambana na Costa Rica wakati Serbia watawakabili Uswis.

Brazil nao watalazimika kupambana kwa nguvu kuhakikisha wapata ushindi katika mchezo wa leo kwani Costa Rica wanashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza na tumeshuhudia timu ambazo hazikupewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwa sasa zikionekana kuwayumbisha miamaba wa soka Duniani.

China kuadhimisha tamasha la ulaji nyama ya mbwa
Kiwango cha Rakitic chaivutia Man Utd