Kiwango cha juu kilichoonyeshwa na kiungo wa timu ya taifa ya Croatia na klabu ya Barcelona, Ivan Rakitic kimeonekana kuzidi kuivutia klabu ya Manchester United ambayo imekuwa ikimnyemelea kiungo huyo kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa chombo kimoja cha habari nchini Hispania (Diario Gol) kimeripoti kuwa kocha wa Man Utd, Jose Mourinho yuko tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 35 ili kupata huduma ya kiungo huyo msimu ujao.

Rakitic aliichezea Barcelona jumla ya michezo 55 msimu uliopita akiisaidia klabu hiyo kunyakua ubingwa wa ligi kuu ya Hispania La liga na katika mchezo wa michuano ya kombe la Dunia uliopigwa jana kiungo huyo alipachika bao moja katika ushindi wa mabao 3-0 ambao Croatia iliupata dhidi ya Argentina.

Tayari Manchester United wamekamilisha usajili wa baki wa kulia kutoka FC Porto, Diogo Dalot na kiungo Mbrazili Fred.

Brazil, Nigeria yatawakuta ya Argentina leo?
Lil Kim aamsha tena bifu na Nicki Minaj