Leo Mei 24, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amepokea Taarifa ya Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza mchanga ulio katika makontena ya mchanga wa madini (Makinikia) yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini Tanzania.
Mara baada ya kupokea ripoti hiyo Rais Magufuli amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo kujitadhimini na bila kuchelewa kuachia madaraka.
“Nimempenda sana Prof. Muhongo, lakini pia ni rafiki angu, lakini kwa hili akae ajifikiria na bila kuchelewa aachie madaraka”
Rais Dkt. Magufuli pia amevunja Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, pia ameagiza sheria kuchukuliwa dhidi ya wajumbe wa bodi hiyo kuanzia leo.
Aidha, Rais Magufuli ameelezwa kusikitishwa na taarifa hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa imeonyesha ni jinsi gani nchi imekuwa ikiibiwa mimiolini ya fedha kama ambavyo ripoti hiyo imeeleza.
Tazama hapa video