Wabunge wa bunge la Uganda, baada ya siku tatu za majadiliano mazito na mvutano wamepitisha sheria kikatiba inayomtaka mgombea wa Urais kugombea nafasi hiyo hata akiwa na miaka zaidi ya 75.
Kupitia kupitishwa kwa katiba hiyo, Rais wa sasa Yoweri Mseveni ana haki kikatiba kugombea nafasi ya Urais kwa awamu ya sita na kuitawala nchi hiyo milele.
Ambapo kupitia majadiliano hayo yaliyofanyika takribani siku tatu kumetokea vurugu mbalimbali kufikia makubaliano hayo yakiwemo wabunge wa upinzani kutoka ndani ya ukumbi wa majadiliano, wabunge wengine sita kufukuzwa ukumbini kutokana na kupinga muswada huo.
-
NEC yashangazwa na mwenendo wa Chadema
-
Video: Waliouza Airtel wakalia kaa la moto, Chadema yajitosa Singida Kaskazini
Hata hivyo muswada huo umepitishwa baada ya kura za maoni kupigwa.
Ambapo Spika wa Bunge hilo, Rebecca Kadaga ametangaza matokea hayo, upinzani waliibuka a kura 61, huku waliounga hoja hiyo wameibuka na kura 315 na kuufanya mswada huo kupitishwa na kuingizwa katika katiba.
Aidha sheria hiyo imeenda sambamba na sheria inayowataka wabunge kuwa na kikomo baada ya kuongoza mfululizo muda wa vipindi viwili.