Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini kupitia tiketi ya Chadema, John Heche ameitaka serikali kuwa mfano mzuri kwa kutoa takwimu za ukweli na kwamba takwimu nyingi si za kweli na inapaswa kushughulikiwa.  
 
Ametoa maoni yake kupitia ukurasa wake wa twitter ikiwa ni siku moja baada ya Rais Dkt. Magufuli kutoa onyo kwa watu wasiohusika kutoa takwimu kufanya kitendo hicho na kuagiza mamlaka husika kuwashughulikia watu hao.   
 
“Serikali inatakiwa kuwa mfano mzuri kwa kutosema takwimu za uongo, lakini tukianzia kwenye takwimu zinazotolewa kuhusu ukuaji wa uchumi, idadi ya viwanda na mengine mengi nafikiri inatakiwa serikali yenyewe ndio ianze kushughulikiwa kwanza,”amesema Heche  
 
 Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli amewataka wananchi kuwa makini na masuala ya takwimu na kuwapuuza watu ambao wanasema vyuma vimekaza ili hali watu wa Takwimu wanasema vyuma vimefunguka na kwamba mtu akikosea kutoa takwimu ameichafua nchi.
 
  • Bashe atuma salaam kwa makocha CCM
 
  • Wasira: Katiba mpya imenibeba
  • Msando alamba dili CCM

Naibu Waziri Mkuu Uingereza afutwa kazi
Bunge la Uganda laondoa kikomo cha umri wa kugombea urais