Aliekuwa Jaji Mstaafu , na mwanasheria mkuu wa kwanza Mtanzania Mark Bomani amefariki dunia .
Taarifa toka kwa mtoto wa marehemu , Andrew Boman zinasema kuwa jaji Boman amefariki usiku wa kuamkia leo Septemba 11, 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Boman alihudumu kama mwanasheria mkuu wa kwanza wa Tanzania kutoka 1965 hadi 1976, ni mwanasheria mkuu wa kwanza kuzaliwa ardhi ya Tanzania na pia kutoka visiwani zanzibar
Bomani atakumbukwa kwa kutumikia serikali ya Tanzania na mataifa mengine , alikuwa mshauri mwandamizi wa sheria katika umoja wa mataifa kati ya 1976 NA 1990, Akifanya kazi kuelekea uhuru wa Namibia ,na kubuni mfumo huru wa sheria kwa nchi hiyo .
Bomani alikuwa na uzoefu mkubwa wa mazungumzo ya kimataifa na pia alikuwa masaidizi mkuu wa mwalimu julius Nyerere na Nelson Mandela juu ya mazungumzo ya amani wakati wa vita ya raia wenyewe kwa wenyewe nchini Burudi .
Marehemu Mark Boman alizaliwa 22 Oktoba 1943 (76) katika eneo la Wete ,Pemba, Zanzibar na alipata nafasi ya kusoma chuo kikuu cha makerere Uganda .
Pumzika Kwa amani Mark Bomani.