Viongozi wa mataifa saba yanayopakana na bahari ya Mediterenia (EuroMed7), wamesema wako tayari kuunga mkono vikwazo vya umoja wa ulaya (EU), dhidi ya Uturuki iwapo itapuuza mazungumzo ya mvutano katika eneo la Mashariki mwa bahari hiyo

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ndiye mwenyeji  wa viongozi wa mataifa mengine sita ya Umoja wa Ulaya yanayojumuisha Ugiriki ambayo ni mpinzani wa Uturuki katika kanda hiyo.

Macron amesema kuwa taifa hilo mshirika wa jumuiya ya kujihami ya NATO sio mshirika tena katika eneo la Mashariki mwa bahari ya Mediterenia na kwamba raia wake wanastahili mambo tofauti kinyume na vile serikali hiyo inavyofanya kwa sasa.

Macron ameongeza kuwa mkutano ulikuwa ni wa nia njema kwa mataifa hayo dhidi ya Uturuki.

Lissu: tujiandae kwa Oktoba 28
Buriani Mark Bomani